Kamati Kuu ya Chama cha chadema imemaliza Vikao vyake jana January  19 , 2018 na imefanya uamuzi wa kushiriki kwenye uchaguzi mdogo wa majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Februari, 2018.

Baada ya uamuzi huu kufanyika , Kamati Kuu imewateua wagombea wa Majimbo hayo kama ifuatavyo;

1. Jimbo la Kinondoni ameteuliwa Mhe. Salum Mwalim Juma

2. Jimbo la Siha ameteuliwa Bwana Elvis Christopher Mosi

Wagombea wote wameshachukua fomu za uteuzi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo husika na watazirejesha kesho Jumamosi tarehe 20 Januari 2018 , kwa ajili ya uteuzi.

Imetolewa Leo tarehe 19 Januari, 2018.

John Mrema – Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top