Mzanzibari Said Omar maarufu Sugu  Mkaazi wa tomondo Wilaya Magharib B  amefanikiwa  kuunda Helkopta ambayo ameionesha  leo katika  viwanja vya maisara Mjini Unguja huku akisubiri  kibali kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini TCAA.

Amesema  amechukua hatua ya kuunda helkopta  akiwa na lengo la kuuonesha umma  uwezo wake wa ubunifu wa vifaa vya  moto ambapo hapa nchini hamna utaalamu  huo.



Akizungumzia  kuhusu   utengenezaji wa helkopta hiyo amesema  imemugharimu  zaidi ya Shillingi Milioni saba  hadi kukamilika kwake na imechukua  miaka minne tokea 2015 hadi 2018  katika  utengenezwaji wake.

Amesema helkopta hiyo inavifaa   vyote  muhimu   vinavyohitajika kuwemo ndani ya helkopta ikiwemo mashine za kisasa, life jaketi, vifaa  muhimu ambavyo vinavyohitajika wakati wa safari.


Ubunifu  huo wa Mr sugu si mara ya kwanza  kubuni vifaa vya moto bali  hii ni awamu ya tatu ambapo awali miaka ya nyuma  alibuni Baluni ya kuruka hewani iliyochukua abiria, Gari ambapo alizawadiwa na serikali Shilingi Milioni Mbili  na hivi sasa amebuni helkopta hiyo ambayo  iliyomugharimu  zaid ya Milioni 7,chanzo Zanzibar 24


Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top