WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti likiwemo la mtoto wa miaka miwili, alietumbukia kwenye hodhi la maji.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Madema, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Mgharibi Unguja,Haji Abdalla Haji, alisema tukio la kwanza lilitokea Januari 24 mwaka huu saa 5.00 asubuhi ambapo Somon Ibrahim Kafula (2) mkaazi wa Chukwani  alifariki dunia baada ya kutumbukia kwenye hodhi la maji.

Alisema marehemu alikuwa anacheza ndani ya nyumba yao karibu na hodhi ndipo alipotumbukia na kufariki.

Alisema baada ya tukio hilo mwili wa marehemu ulikimbizwa hospitali ya Mnazimmoja kwa uchunguzi kisha kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi.

Kuhusiana na tukio hilo Kamanda Haji alitoa wito kwa wazazi kuwa makini na kuangalia nyenendo za watoto wao wanapocheza ili kuepuka ajali.

Katika tukio jengine Tausi Mussa Alawi (13)  mkaazi wa Migombani alifariki baada ya kuripukiwa na kopo la mafuta lililokuwa limewekwa karibu na jiko wakati akipika.

Tukio hilo lilitokea Januari 22 mwaka huu saa 10.00 jioni.

Alisema marehemu alikuwa nyumbani kwao akipika na kopo la rangi  ya mafuta  lilikuwa karibu na jiko, ndipo liliporipuka na kummwagikia mwili mzima.

Alisema kabla ya kifo alikimbizwa hospitali ya Mnazimmoja kwa matibabu lakini kutokana na hali yake kuwa mbaya alifariki wakati akitibiwa.chanzo Zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top