SHIRIKISHO la Soka Afrika CAF limetangaza majina ya waamuzi watakaochezesha mchezo  wa  kombe la Shirikisho baina ya timu ya Zimamoto ya Zanzibar na Wolaitta Dicha SC ya Ethiopia.

Mchezo wa awali utapigwa uwanja wa Amaan Febuari 11 saa 10:00 jioni,  ambao utachezeshwa na  waamuzi Hafiz Abdelghani Alamen, Omer Hamid Mohamed Ahmed,Abdelgabar Mohamed Abdelgabar, mwamuzi wa hakiba Adel Mukhtar Adam wote kutoka Sudan, wakati kamishina wa mchezo ni  Maxwell Mtonga kutoka Malawi.

Mchezo marudiano  utachezwa  katika uwanja wa ‘Hawass International Stadium Febuari 22 saa 10:00jioni.

Mchezo huo utachezeshwa na mwaamuzi wa kati Souleiman Ahmed Djamal akisaidiwa na Salah Abdi mohamed  na Liban Abdourazak Ahmed, mwamuzi wa hakiba Mohamed Diraneh Guedi wote kutoka Djibouti na kamishna wa mchezo Lewis Blaze Madeleine kutoka Shelisheli.

Kwa upande wa klabu bingwa wawakilishi wa Zanzibar JKU wataanza kucheza nyumbani na Zesco United ya Zambia Febuari  10 majira ya saa 10:00 jioni.

Waamuzi watakaochezesha mchezo huo ni  Jiny Claudio Shimiwe, Teugeni Ngadigimana, Amros Hakizima ,Rusindana Musoro wote kutoka  Rwanda, mechi kamishna atakuwa Seleiman John Apapane kutoka Lesotho.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa Febuari 21 huko Zambia saa 09:00 za mchana.
Waamuzi wa mchezo huo ni Tulani Sibanze, Sefino Sumalo, Zamani Tula na Mbolsiene Eluati Faduze wote kutoka Switzerland, mechi kamishana ni  Gail Magoena kutoka Afrika Kusini.

Wamuzi wanne wa Zanzibar waliochaguliwa na CAF kusimamia mashindano klabu bingwa na Kombe la Shirikisho, ambapo waumuzi hao wanaume wawili wakiwemo Mzee Zamu Ali na Muhsin Ali Kamara na wanawake wawili ambao ni Laila Said Abdallah na Asha Nassor Sultan,chanzo Zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top