ZIARA YA MHE LOWASSA IKULU.

Kumekuwa na waraka na taarifa nyingi za kupotosha UMMA kuhusu ziara ya Mhe. Edward Lowassa kwenda Ikulu na nyingine zikisemwa zimetoka kwa msemaji wake, taarifa zote hizo siyo kweli na wala siyo rasmi kutoka ofisini kwa Mh.Lowassa.

Baada ya ziara ile, Mhe Lowassa alikutana na Mwenyekiti wa Chama chake, Mhe Freeman Mbowe na Kumpa mrejesho wa yaliyojiri Ikulu.

Kumekuwa na taarifa nyingi kwenye mitandao zikiwemo kufunguliwa kwa akaunti mbalimbali feki, taarifa zote hizo zipuuzwe kwani zina lengo la kupotosha kwa malengo wanayoyajua wapotoshaji hao pamoja na mawakala wao.

Taarifa rasmi zitatolewa kwa njia rasmi na watu wenye mamlaka hiyo.Poleni kwa usumbufu wote, Mwisho tutayashinda haya kama tulivyoshinda mengine kwa umoja wetu.

Imetolewa na

Aboubakary Liongo
Msemaji Rasmi wa Mhe Edward Lowassa.
 

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top