BAADA ya kusimama kwa muda wa wiki mbili kupisha mashindano ya            Kombe la Mapinduzi,  ligi kuu soka Zanzibar kanda ya Unguja itarejea tena dimbani  leo.

 

Akizungumza na vyombo vya habari, Msemaji wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ali Bakari ‘Cheupe’, alisem, ligi hiyo itaanza na michezo ya viporo ambayo  haikuchezwa wakati wa maandalizi ya timu ya taifa ya Zanzibar Heroes.

 

Pia alisema kuwa michezo mingine  itahusisha mechi ambazo hazikuwahi kuchezwa kupisha mashindano ya Kombe la Mapinduzi, hivyo mechi hizo baadhi zitazigusa timu zote 14, na michezo mingine itahusisha timu za JKU , Taifa Jang’ombe, KMKM, Kipanga Black Sailor na Chuoni.

 

Hivyo kamati tendaji ya chama cha soka ZFA  imekaa kikao chini ya mkurugenzi wa ufundi wa chama hicho, Abdulghani Msoma, na kuamua kuwa ligi hiyo itaendelea tena kesho Alkhamis.

 

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa siku hiyo kutachezwa michezo miwili, wakati wa saa 8:00 mchana JKU na Charawe , wakati saa 10:15 jioni kutakuwa na dabi ya Jang’ombe timu za Taifa Jang’ombe na Jang’ombe boys zitapepetana.

 

Michezo hiyo itaendelea tena Ijumaa Januari 19  kutafanyika mchezo baina ya Kipanga na KMKM saa 10:15 jioni, Jumapili Januari 21 Zimamoto itacheza na JKU saa 8:00 mchana,  na saa 10 jioni Kilimani City itakwaruzana Taifa Jang’ombe.

 

Jumatatu Januari 22 mechi hizo za vipiro zitamalizika kwa kupigwa michezo miwili ambapo saa 8:00 mchana KMKM watacheza na Chuoni, wakati saa 10:15 jioni Black Sailor watakutana na Kipanga.

 

Alisema kuwa kumalizika kwa michezo hiyo itazifanya timu zote 14 kukamilisha  michezo 11 kila mmoja.

 

Alifafanua kuwa  kuanzia Februari  7 ligi  hiyo itasimama hadi Febuari 13, ili kupisha michezo ya kimataifa itakayo wahusisha JKU ambayo itacheza ligi ya mabingwa na Zimamoto itacheza kombe la Shirikisho, zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top