MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchimi Zanzibar (ZIPA) na Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe, kuhakikisha muwekezaji aliyepewa mradi wa hoteli ya Bwawani  anaufanyia matengenezo ya haraka ukumbi wa mikutano wa Salama.


Alisema agizo hilo lazima litekelezwe ndani ya kipindi cha miezi mitatu kuanzia kwani ukumbi huo  ni wa kijamii na wananchi wanaupigia kelele kutokana na kushindwa kutoa huduma.
Alitoa agizo hilo alipofanya ziara kutembelea miradi ya uwekezaji  katika maeneo mbali mbali ndani ya Mkoa Mjini Magharibi.

Alisema wananchi wanahoji kuchelewa kwa mradi huo ambao walitegemea kuleta matumaini kwa jamii pam oja na kuongeza mapato ya Taifa yatayokwenda sambamba na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wengi nchini.

Alisema ukumbi wa Salama wa ndio pekee unatoa huduma za kijamii kwa watu wenye kipato cha chini jambo ambalo kusitisha huduma zake kunaendelea kuwapa usumbufu wa maeneo ya kuendesha shughuli zao za Kijamii ikiwemo harusi.

Naye Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud, alisema wananchi wa Mitaa iliyomo ndani ya Wilaya ya Mjini hivi sasa wanalazimika kutafuta Ukumbi wa kufanya shughuli zao za Kijamii katika maeneo ya mbali ikiwemo Meli Nne Saccos.

Alisema kitendo hicho mbali ya kuleta kero na usumbufu lakini pia kinachangia na kuongeza gharama zisizo na tija ambazo zisingewakumba iwapo Ukumbi wa Salama ungekuwa ukiendelea kutoa huduma kama kawaida.

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe, Said Sarboko Makarani alimueleza Balozi Seif r kwamba Muwekezaji wa mradi wa hoteli ya Bwawani bado ana nia ya kuendelea na ujenzi wa Mradi huo wa Kitalii.

Alisema kwa mujibu wa muongozo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezji wa Mji Mkongwe Muwekezaji huyo hawezi kuanza na ujenzi wa majengo mapya katika eneo hilo.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top