Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne Muliro, amesema wanafikiria kuanza kuwakamata wanaume ambao wanaonunua wanawake wanaojiuza 'Machangudoa' katika mitaa mbalimbali ya Kinondoni.


Kamanda Muliro ameyasema hayo leo Ijumaa Desemba 29,2017 kwenye kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio ambapo amesisitiza kuwa, kufanya hivyo itasaidia kupunguza wateja na hivyo wadada hawatajiuza tena kwasababu watakosa wateja.

“Nafikiri kama wanaume wangekubali kutokwenda kwa hao madada poa hiyo biashara ingekufa sasa nafikiri badala ya kuwakamata tu hao wadada, wasishangae kwa mkoa wa Kinondoni tukaanza kuwakamata hao wanaume na kuwafikisha mbele ya sheria”, amesema Kamanda Muliro.

Aidha Kamanda Muliro amesema Jeshi la polisi Kinondoni limejipanga kuhakikisha wananchi wakiwemo wafanyabiashara wanafanya shughuli zao kwa amani na usalama kwenye sikukuu ya mwaka mpya.

Chanzo, Malunde

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top