Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na kamati Kuu ya kufuatilia mali za Chama cha Mapinduzi(CCM) aliyoiunda hivi karibuni mjini Dodoma.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Mwenyekiti wa kuhakiki mali za chama hicho, Dr. Bashiru Ally amesema kuwa mambo makubwa walioyazungumza katika mkutano huo ni sababu za kuunda tume hiyo, kazi zake na faida zake kwa chama na kwa nchi.

“Tumekaa kuzungumza na Mwenyekiti karibia masaa mawili, kutueleza matarajio yake, sababu za kuunda tume hii, kazi zake na faida zake kwa chama na kwa nchi. Kwahiyo tumezungumza nae ametukabidhi vitendea kazi na taarifa mbalimbali na ametualeza kwamba kazi yake ni kuhakikiki mali zote za chama kwashirikiana na wana chama na wale wanaoshirikiana na wanachama kuzitumia hizo mali kama wapangaji au wasimamizi,” amesema Dr. Bashiru.

“Tumekuwa na mkutano mzuri kama wajumbe wote tisa na tumeanza kazi rasmi leo na makisio yetu tunaweza tukatumia labda mwezi mmoja lakini hiyo inategemea na ushirikiano tutakao upata , kwahiyo kubwa ninalo lisema kwa niaba ya tume ni kuomba ushirikiano.”

chanzo, Zanzibar 24

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top