Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Uwekezaji Doroth Mwaluko amesema kufanyika
Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC) kutasaidia kubadilishana taarifa
za uzoefu pamoja na kupunguza athari za Maafa .
Hayo aliyasema
wakati wa Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi huko katika Ukumbi wa
Madinat Al- Bahr Mbweni Zanzibar
Alisema kikao
hicho kitasaidia kuwa na jukwaa la kubadilishana uzoefu wa kiutendaji kwa lengo
la kutekeleza kwa ufanisi shughuli za usimamizi wa maafa
Aidha alisema
Mkutano huo umekuja katika kipindi ambacho nchi nyingi wanachama katika ukanda
huu zimekuwa zikiathiriwa na majanga ya asili ya mara kwa mara na kusababisha
madhara makubwa .
Nae Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Abdalla Hassan Mitawi amezishauri Nchi
wanachama wa SADC kushirikiana katika kukabiliana na maafa kwa hatua watazozichukua
ili kudhibiti athari za kimazingira zinazoweza kujitokeza.
Amesema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari inatumia boti za uokozi pamoja na
ndege zisizokuwa na rubani kwa kuimarisha shughuli za uokozi hata hivyo
inahitaji ushirikiano unahitajika kutoka Nchi nyengine.
Mkutano huo wa Ngazi za Makatibu Wakuu
unaandaa Ajenda zitazojadiliwa katika Mkutano wa Mawaziri unaotarajiwa
kufunguliwa siku ya Ijumaa ijayo na Mgeni Rasmi wa Mkutano huo ni Rais wa ZanzIbar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Madinat
Al Bahr
Kauli mbiu
ya mkutano huo ni “USHIRIKI WA KISEKTA KWENYE KUPUNGUZA MADHARA YA MAAFA NI
NJIA BORA YA KUIMARISHA USTAHAMILIVU KATIKA UKANDA WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA
YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA” ( SADC)
Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye
dhamana ya uongozi wa Maafa kwa Nchi
Wanachama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa Nchi Wanachama 15 kati ya 16 zitashiriki Mkutano
huo .
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment