*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*

*TAARIFA KWA UMMA*

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi Wateja wake wote wa Mikoa iliyounganishwa katika gridi ya Taifa kwa kukosa huduma ya umeme leo Alhamisi, Septemba 27, 2018, majira ya Saa 7:42 Mchana.

*Sababu* hitilafu katika transfoma ya 220/33 kV ya kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme cha Kidatu (Kidatu switch yard).

Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na jitihada za kurejesha umeme katika hali yake ya kawaida.

Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz,

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

 Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

*IMETOLEWA NA:*
OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top