Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amewataka Wafanyakazi wa Wakala wa matukio ya Kijamii Zanzibar kutoa huduma zinazostahiki kwa Wananchi ili kupata taarifa sahihi katika kazi zao.


Dkt Shein ameyasema hayo leo septemba 4, 2018 Dunga Mkoa wa kusini Unguja wakati akizindua Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar.

Alisema ili kupata taarifa sahihi na kujua idadi ya watu lazima kujenga masharikiano makubwa baina yao  na Wananchi.

Alisitiza Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inahitaji takwimu sahihi hivyo Wafanyakazi nilazima kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya sheria, kanuni na uadilifu.

Aidha aliwataka wafanyakazi hao kuelimisha jamii juu ya suala zima la kujisajili katika matukio ya kijamii kwalengo la kupambana na changamoto zitazojitokeza.

“Katika kazi hii changamoto mbalimbali zitajitokeza hivyo ni muhimu kupambana na changamoto hizo kwa kuzifanya ziweze kuleta mafanikio” alisema Rais Shein.

Hata hivyo Rais wa Zanzibar alitoa wito kwa wananchi na wageni  kutumia vizuri fursa hiyo na kila mmoja awe tayari kutoa taarifa sahihi zinazomuhusu.

Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa  na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir alisema kuwa sheria iliyowekwa inataka matukio yote ya kijamii ni lazima yasajiliwe .

Alisema kuwa kila kitu kimekamilika na tayari kuanza rasmin kwa kufanya usajili kwa Wakaazi wa Zanzibar pamoja na wageni waliokuwepo Zanzibar.

Alilisisitiza kuwa upo umuhimu mkubwa kwa wageni kwa upande wao kusajiliwa kwani wanasehemu yao tofauti na wenyeji wa Zanzibar.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top