Jamii ya watu wenye ulemavu wilaya ya kati mkoa wa kusini Unguja wameiomba Serikali kuwajengea na kuboresha miundombinu rafiki katika upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii.


Wakizungumza katika mkutano maalumu  wa kujadili matatizo wanayokabiliana nayo watu wenye ulemavu  katika maeneo yao ikiwa ni muendelezo wa kutekeleza mradi wa Paza kushirikiana na wanaharakati na  Jumuiya za maendeleo katika vijiji husika katika Nyanja za Elimu , Afya, kilimo, mazingira  na maji.



Wamesema wanakabaliana na changamoto nyingi  katika kuzifikia huduma muhimu za kijamii kama vile upatikanaji wa Maji safi na salama,afya na  Elimu jambo ambalo linawafanya kuwa nyuma kimaendeleo na kubaki kuwa omba omba.


“sisi watu wenye ulemavu ndio watu duni tusiothaminika katika jamii zetu kutokana kukosa huduma muhimu ambazo zingepelekea sisi kujiendeleza na kujiinua kimaisha na kuacha kuwa tegemezi” alisema Yunusi Kassim Mwenyekiti jumuiya ya watu wenye ulemavu wa macho mkoa wa kusini Unguja.


Nae Afisa ufuatiliaji na tathimini kutoka halmashauri ya wilaya ya kati Mohamme Khatibu Mohameed amekiri kupokea changamoto zinazowakabili walemavu mkoa wa kusini Unguja na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi kwa kuwakutanisha na Serikali  ili nao waishi katika usawa kama jamii ya watu wengine.


Kwa upande wake Daktari Dhamana kutoka halmashauri ya kati amesema kutokuwepo miundombinu Rafiki katika vituo vya afya na skuli nyingi katika wilaya ya kati kunatokana na majengo hayo kuwa yamejengwa kwa muda mrefu.


Mkutano huo wa siku moja umeandaliwa na Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA kwa kushirikiana na Jumuia ya Waandishi wa habari za maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA),Jumuia ya Kuhifadhi maliasili za asili Pemba NGERANECO kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

 

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top