Mwashungi Tahir       Press Club Zanzibar    

WAANDISHI  wa habari nchini wametakiwa kufuatilia kwa upeo mkubwa katika masuala ya kijinsia kutokana na jamii kukabiliwa na mabadiliko makubwa ya kimaadili na kuweza kuonekana mwanamke kama ni mtu duni asiye na uwezo wa kufanya jambo lolote kwenye jamii.


Hayo aliyasema mwezeshaji kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Haura Shamte wakati alipokuwa akiwasilisha mada ya Vyombo vya Habari na Jinsia kwenye ukumbi wa watu wenye ulemavu ulioko Kikwajuni Welesi .


Alisema kwa kipindi hichi kuna hali nzito  katika masuala ya udhalilishaji wa kijinsia  ambapo jamii yote imekuwa na taharuki  na kuwataka waandishi wa habari kuwa na  ufuatiliaji  kwa nguvu zao zote masuala haya kwa undani zaidi.


“Sasa hivi wimbi kubwa tulilokuwa nalo la udhalilishaji wa kijinsia hivyo nawaomba waandishi wa habari watumie kalamu zao kwa kufatilia masuala haya ili yasiendelee”. Alisema mwezeshaji huyo.


Pia alisema kutokana na wimbi hili liliopo la udhalilishaji kumejitokeza mabadiliko mengi ya kimaadili hivyo aliwaomba waandishi wa habari kukemea vitendo vy a ukatili wa kujinsia kwani vitendo hivi vinashamiri na kumnyima haki zake mwanamke au mwanamme.


Aidha alisema mfumo dume umeweza kuchukua nafasi kubwa kwa kuona mwanamke hana fursa yeyote ya kujitolea maamuzi katika mambo yake na mwanamme kujiona yeye ndio mwenye maamuzi yote  ya kisiasa , uchumi na hata uongozi.


Sambamba na hayo mkufunzi Ali Haji Mwadini mkufunzi wa masuala ya  habari akiwasilisha mada ya maadili katika kuandika habari aliwataka amewasihi sana kuandika habari zenye maadili na kuwa  zenye kuwa na ukweli na uaminifu.


Pia aliwataka watu wote wapewe haki zao  na kujitahidi kuyalinda maadili ili tuweze kuepukana na athari zitakazoweza kujitokeza kwenye jamii na kuepuka kuegemea upande mmoja.


Nae Afisa program  mwandamizi  Shifaa Said Hassan alisema waandishi wa habari wawe na mchango mkubwa wa kuiandikia jamii  katika masuala ya udhalilishaji  kwa kufuatilia  na kutoa muendelezo na wajue kitu gani kinaendelea hadi kufikia mstakbala mzuri


Nao waandishi wa habari hizo wameahidi kuzifanyia kazi mafunzo waliyopatiwa na kutumia kalamu zao kwa vizuri katika kutoa habari na kupambana kwa nguvu zote katika masuala haya ya udhaliishaji.


Mafunzo haya ya siku mbili yameandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) chini ya ufadhili wa mradi wa kusaidia asasi zisizo za kiserikali Zanzibar(ZANSASP).


 


 


 


 


Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top