Mwenyekiti wa Cuf anayetambuliwa na msajili wa vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Limpumba amemtaka Maalim Seif kufuta kesi alizofungua dhidi ya Chama kutokana na kesi hizo hazina faida na Chama.

Alisema kuendelea na kesi Mahakamani kwa muda mrefu ni kupoteza pesa pamoja na kupoteza muda wa kufanya kazi za uhai wa Chama

Lipumba alitoaka kauli hiyo leo Alhamis huko Malindi Mjini Unguja wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema hatua ya Maalim Seif kufungua kesi ni kitendo ambacho hakitamnugaisha hata kidogo badala yake manufaa zaid yanakwenda kwa mawakili wanaosimamia kesi hizo.

Hivyo alisema ili Maalim na kund lake waepukane na hasara hizo ni vyema wakaachana na kesi hizo ambazo hazina faida kwa maslahi ya ujenzi wa Chama.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top