Kamati teule iliyoteuliwa na mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar baada ya kuivunja kamati tendaji ya ZFA imesema bado inaendelea na mchakato wa Katiba ya ZFA ambayo ndio kazi ya msingi ya kamati hiyo iliyopewa kwenye orodha ya majukumu yao.
Katibu wa kamati Khamisi Saidi amesema bado kamati inaendelea na jukumu lake la kusimamia upatikanaji wa katiba ya ZFA ambayo rasimu yake ipo tayari bado ipo chini ya wanasheria kwa sasa.
Aidha Khamisi Said amesema mchakato wa katiba ndani ya kamati hiyo haiko kimya na kama watu wanavyoona ila sasa bado jopo la wataalamu linaendelea na majukumu yake ya kusimamia chombo hicho muhimu kwenye soka la Zanzibar.
“Tunaunga mkono juhudi zilizofanywa na viongozi wa ZFA waliopita katika kusimamia mpira wa Zanzibar tayari rasimu ya katiba ipo na iko katika marekebisho muda si mrefu italetwa kwa wadau”Alifafanua Khamis saidi.
Kwa Upande mwengine amesema rasimu hiyo bado inatakiwa kufanyiwa marekebisho kwa baadhi ya vifungu na katiba hiyo itakuwa katiba bora ambayo italeta matumaini kwa wadau wa mpira Zanzibar.
“Tunatarajia ikimaliza kazi yetu rasimu hiyo itawafikia wadau wote wa mpira wa miguu na washabiki ikiwemo wachezaji wa zamani na wandishi wa habari kwa lengo la kuona tunatengeneza mpira wa Zanzibar kwa pamoja “Alisema Khamis Saidi.
Mwisho khamisi saidi amesema kamati hii haifanyi kazi na makundi yeyote ya watu wala shindikizo badala yake ipo tayari kushirikiana na mtu yeyote kwenye masuala ya mpira wa Zanzibar ili kuleta umoja kwenye mpira wa Zanzibar.
Post a Comment