Waziri wa Habari Utamaduni na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo amesema Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari wanajukumu la Kufanya kazi kwa kufuata sheria na maadili ya kazi zao ili kuiweka Nchi katika hali ya Amani na Usalama.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru ya Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Ukumbi wa wizara ya Habari Kikwajuni Mjini Zanzbar amesema Vyombo vya Habari na Waandishi wanategemewa sana katika jamii hivyo si vyema kufanya kazi kinyume na maadili yao.
Amesema watakapoendelea kufanya kazi kwa sheria watawawezesha wananchi Kunufaika na haki zao za Msingi na serikali kuweza kutoa huduma Muhimu katika jamii zitakazoimarisha Maendeleo ya Nchi.
Amesema kutokana na umuhimu wao Serikali pia itaendelea kuthamini na Kuheshimu Uhuru wa Vyombo vya Habari pamoja na kuendelea kutoa taarifa zinazohitajika ili kuwawezesha Waandishi kufanya kazi zao kwa weledi.
Aidha ametowa wito kwa waandishi wa Habari kuripoti Sehemu Husika matatizo wanakutana nao wakati wa utendaji wa kazi zao ikiwemo tatizo la mikataba baina yao na waajiri wao ili matatizo hayo yaweze kupatiwa ufumbuzi.
Awali Raisi wa Clabu za Waandishi wa Habari Nchini Tanzania Deogratius Nsokolo amesema licha ya Waandishi wa habari kufanya kazi kwa Kufuata Sheria lakii wamekabiliwa na Matatizo mbalimbali ikiwemo kukosa Mikataba,bima za Afya na Mafao katika Tasisi zao.
Amesema ili Mwandishi wa habari aweze kufanya kazi kwa kuwafikia wananchi ni vyema kwa Vyombo vya Hbari kujali Afya na Mahitaji ya Wandishi wa habari ili Vyombo hivyo viweze kufikia malengo waliyoyakusudia.
Aidha ametowa wito kwa Waandishi wa Habari kuendelea kufanya kazi kwa kwa mashirikiano katika kuwasaidia wananchi kwa kuwakosoa na kuwakumbusha viongozi wa Serikali kujua wajibu wao juu ya kutatua matatizo yanayowakabili Wananchi.
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment