RAISI wa Zanzibar na Meyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein leo ameongoza mamia ya wafanyakazi katika ukumbi wa baraza dogo la wawakilishi Wete Pemba katika kusherehekea siku ya wafanyakazi duniani.

Katika sherehe hizo pamoja na mambo mbali mbali dk Shein amesema kwa wakati huu hataongeza mshahara kwa wafanyakazi wa Serikali kutokana na hali ya uchumi ilivyo.

Amesema kuwa pamoja na kutoongeza mishahara lakini ameahidi pindi wafanyakazi wakifanya kazi kwa kujitolea zaidi na kuingizia mapato zaidi Serikali ataweza kuongeza mishahara hiyo bila ya wasi.

Hivyo amewataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa moyo mmoja wakiamini kuwa serikali yao ipo pamoja nao katika kuhakisha wanafanya kazi katika mazingira mazuri na ya kuvutia.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top