JESHI la Polisi Zanzibar limesema katika kipindi cha miaka 54 ya mungano, Zanzibar inajivunia mafanikio mengi ikiwemo amani na utulivu.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohamed Haji Hassan, alisema visiwa vya Zanzibar vipo salama hatua ambayo imetoa nafasi kwa wananchi kufanya shughuli zao za kijamii na kujiletea maendeleo.

Alitumia fursa hiyo kuitaka jamii kuendeleza amani na utulivu uliopo ili kuzidi kuimarisha maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top