MTOTO mmoja  mwenye umri wa miaka mitatu, amefariki baada ya kuingia kwenye shimo la choo.

Msaidi Mkuu wa Kituo cha Zimamoto Mjini, ASF Ali Muhsin Makame, alisema alimuokoa mtoto huyo baada ya kutafutwa siku nzima bila ya mafanikio.

Mtoto huyo aliefahamika kwa jina la Nayla Hamza Mohammed, ambae alikutwa na mauti hayo wakati akiwa amekutikana katika shimo la choo maeneo ya Kwamtipura wilaya ya mjini Unguja.

Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 12:30 jioni, maeneo ya Kwamtipura,  wakati akiwa katika michezo yake ya kila siku.

Kikosi cha zimamoto na uokozi kilifanikiwa kufika katika eneo la tukio mara tu baada ya kupata taarifa hiyo na kufanikiwa kumpata kwenye shimo la choo akiwa tayari ameshafariki dunia.

Aidha Muhsin, alitoa wito kwa jamii kuwa na tahadhari juu ya watoto wao pale wanapotoka majumbani, kwani itasaidia kujilinda na majanga ya mara kwa mara.

Baba Mazazi wa mtoto huyo, Hamza Mohammed, alielezea kuwa mtoto wake alipotea majira ya jioni na kuchukua juhudi za kuanza kumtafuta huku wakishirikiana na majirani kwa kupeleka taarifa kituo cha polisi na kufanikiwa kumuona siku ya pili akiwa ndani ya shimo la choo.

Nae Sheha wa Shehia ya Kwamtipura, Ameir Suleiman Khamis , aliishauri jamii kuhakikisha wanapojenga makoro wanayafunika ili kujinusuru na majanga hayo.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top