UHABA wa fedha unaoikabili Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni ya vikwazo katika ufikia malengo ya kukua kwa matumizi ya lugha hiyo miongoni mwa nchi wanachama.

Mkuu wa ujumbe kutoka Bunge la Jumyuiya ya Afrika Mashariki, (EALA), Wanjiku Muhia, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya wabunge wa bunge hilo ya kutembelea makao makuu ya Kamisheni ya Kiswahili Afrika, iliyopo  Ecrotanal mjini Unguja.

Alisema ili kazi za kamisheni hiyo zifanikiwe hasa katika utoaji wa elimu ya kutambulika kwa lugha ya Kiswahili, hakuna budi kuwepo bajeti ya kutosha ambayo itaweza kukidhi mahitaji yote ya ufanikishaji wa shughuli za msingi zinazofanywa na kamisheni hiyo.

Alisema pamoja na kamisheni kuandaliwa kwa bajeti lakini bajeti hiyo haitimii kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kuchelewa kwa michango kutoka kwa nchi wanachama na wahisani.

Alisema pamoja na hali hiyo, bunge la Afrika Mashariki litandelea kupigania kwa nguvu zote kuhakikisha bajeti ya kamisheni hiyo inapatikana kikamilifu ili kufikia malengo yaliokusudiwa.

“Kwa kuwa sisi tumechaguliwa hivi karibuni,  tumeliona hilo ila kwanza tumeanza ziara ya kutembelea ofisi za kamisheni ya Kiswahili ili kujua changamoto nyengine mbali mbali ambazo sisi kama wabunge tunaweza kupambana nazo,”alisema.

Alisema mbali ya tatizo la kutoenea lugha hiyo, lakini ndani ya jumuiya hiyo kuna kazi nyingi zinahitajika kufanyika ikiwamo suala la biashara kwa lengo la kuhakikisha kuna haki sawa kwa nchi zote za Afrika Mashariki bila ya kuwepo ubaguzi.

Mbunge Maryam Ussi Yahya, ambaye pia ni mjumbe kamati ya fedha ya EALA, alisema ili kamisheni ya Kiswahili ifanikiwe katika kufanya kazi zake inahitaji zaidi ya dola za Marekani milioni nne.

“Ila katika bajeti inaonesha kuwa kwa mwaka huu wa fedha unaomaliza zimepatikana dola za Marekani 1.5 milioni kiwango ambacho hata nusu hakijafikia na kidogo sana katika uendeshaji wa shughuli za kukitangaza Kiswahili,”alisema.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top