MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema serikali ya mkoa wake itatoa ushirikiano ili kuhakikisha shilingi milioni 72 za matumizi ya ijitmai ya kimataifa inayotarajiwa kufanyika Ole Kianga Mkoa wa Kusini Pemba zinapatikana kwa wakati.

Aliyasema hayo wakati akizindua shughuli ya ijitmai inayotarajiwa kufanyika Machi 16 mwaka huu, hafla iliyofanyika makao makuu ya Fiy-sabil-llahi Tabligh markaz Fuoni wilaya ya magharibi ‘B’ Unguja.

Alisema atahakikisha anakuwa karibu na viongizi wa markaz kwa kushirikina na waumini wa dini ya kiislamu ili kutimiza  wajibu wao wa kuungana katika kuchangia shughuli za dini.

Hivyo aliwaomba waumini wa dini ya kiislamu wenye uwezo kujitokeza kuchangia huku akihimiza umoja, upendo na  kusaidiana miongoni mwao.

Aliupongeza uongozi wa Fiy-sabil-llah-tablih Markaz Zanzibar kwa juhudi zao mbali mbali wanazochukua za kuisimamia dini ya kiislamu na kuwajaza imani waumini wa dini hiyo katika ujenzi wa jamii iliyo na maadili.

Naibu Katibu Mkuu wa Markaz hiyo, Mrisho Khamis, alisema lengo la ijitmai hiyo ni kuwakutanisha pamoja waumini wa dini ya kislamu kutoka mataifa mbali mbali ili kukumbusha umuhimu wa kumcha Mwenyezi Mungu.

Mapema Amir Mkuu wa markaz hiyo, Ali Khamis Mwinyi, alisema faida ya ijitmai hiyo ni kupata ukukumbusho wa kiimani katika elimu ya dini ya kiislamu na  kuimarisha elimu ya maadili pamoja na elimu ya malezi na makuzi katika uislamu.

Alisema markaz yao imeanzisha skuli ya Raudha Academy ambayo tangu kuanzishwa kwake imepata maendeleo makubwa ya kitaaluma.


Katika uzinduzi huo, kumefanyika harambe ya kuchangia shughuli za ijitmai hiyo  ambapo zaidi ya  shilingi milioni 1.5 zilikusanywa ambapo Mkuu wa Mkoa alichangia shilingi milioni moja na  kuahidi kuwapatia msada watoto yatima wanaolelewa kituoni hapo.
chanzo Zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top