UONGOZI wa hospitali ya Mnazimmoja, umesema unatarajia kuajiri kampuni ya usafi ili kuhakikisha huduma za usafi katika zinaimarishwa.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi utawala wa hospitali hiyo, Abubakar Khamis Hamadi, wakati akizungumza na Zanzibar Leo.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuiweka hospitali katika mandhari nzuri licha ya kuwepo wafanyakazi walioajiriwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Alisema tayari zabuni ya kuipata kampuni ya kufanya kazi hiyo imetangazwa na kampuni imepatikana.

Alisema kinachosubiriwa ni makubaliano ya gharama ya kufanya kazi hiyo kati ya wizara na kampuni husika.

Aliwaomba wananchi kudumisha usafi ili kujikinga na maradhi mbali mbali yanayosababishwa na uchafu.

Alisema hospitali ya Mnazimmoja ni kubwa hivyo hawana budi kuimarisha huduma ili iendane na hadhi yake.
chanzo Znzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top