WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheir, amewaomba  wananchi wa kijiji cha Pujini Wilaya ya Chake Chake, kukitunza kituo cha usindikaji mazao ili malengo ya kuanzishwa kwake yaweze kutimia.

Alisema hayo Pujini wakati akifungua jengo la kituo cha kusindikia mazao na elimu kwa wakulima, ikiwa ni mfululizo wa shamra shamra za miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Aliwataka wananchi kukitumia ipasavyo kituo hicho ambacho serikali imefanya jitihada kubwa ya kukijengea  kwa gharama kubwa.

Aliwatanabahisha wananchi kuwa serikali yao bado itaendelea kuwapelekea maendeleo bila ya kujali itikadi zao za kisiasa au maeneo wanayotoka.

Aliipongeza Wizara ya Kilimo kwa juhudi ilizochukua kuhakikisha kituo hicho kinamalizika mapema licha ya kasoro zilizojitokeza kutokana na muda ambao ulipangwa kumalizika.

Aliwataka maofisa ugani kutokaa maofisi na badala yake waende kwa wakulima  kujua matatizo yanayowakabili na kuyapatia ufumbuzi.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Joseph Abdalla Meza, alisema kituo hicho kitawahudumia wananchi kutoka sehemu zote za Pemba ambapo jumla ya shilingi 200 milioni zimetumika.

Alieleza jengo hilo ambalo ni la kisasa  pia litatumika kutoa elimu kwa wakulima, wajasiriamali pamoja na wananchi ili waweze kuhifadhi mazao yao baada ya mavuno,chanzo Zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top