Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kuwa Kamishna wa Madini.
Rais ametangaza uteuzi huo leo Jumatatu Januari 8, 2018 alipokuwa akitoa
hotuba fupi mara baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa
Naibu Waziri wa Madini.
“Nimesikia tatizo ni kamishna wa madini, sasa nimeamua kumteua kamishna
mpya wa madini, jina lake linaanza na Prof. Shukrani Elisha, huyo
atakuwa ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa madini.
“Mambo ya hovyo ni mengi mno, nilipotembelea bandarini niliunda katume
kasirisiri hivi, kwa kulihusisha Jeshi la Wananchi, TISS na Polisi.
Yanayogundulika huko ni ya ajabu, kuna hadi simenti za zamani sana, yapo
makontena bandarini na pale Ubungo.
“Mimi sio mwanasiasa mzuri wa kubembelezabembeleza, nikitoka mimi
mtapata wakubembeleza, ila mimi nataka kabla ya Ijumaa regulations
(kanuni za sheria ya madini) ziwe zimesainiwa. Pro Kabudi nendeni
mkazifanyie kazi, tafuta watu wa kukusaidia na mkamalize hayo,” alisema
Magufuli.
Kamishna aliyekuwepo, Mhandisi Benjamin Mchwampaka amehudumu katika
nafasi hiyo kwa siku 263 tangu alipoteuliwa mpaka leo uteuzi wake
ulipotenguliwa na Rais magufuli.
Aidha rais Magufuli amewataka watendaji wote wa Wizara ya Madini kuchap
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment