RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein atawatunuku Nishani ya Mapinduzi wanamichezo na wasanii mbali mbali Januari 11 Ikulu Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu inaeleza kuwa Dk. Shein atawatunuku Nishani hizo kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 4 cha Sheria ya Mambo ya Rais Namba 5 ya mwaka 1993.

Wanamichezo ambao watakaotunukiwa Nishani hizo ni Said Matar Mwinyi , Hafidh Badru Juma aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’,Marehemu Maj. (mst) Mosi Kassim Mosi, LTCol. (mst) Songoro Abdi Waziri.

Wengine ni Salum Nassor Said (Mkweche),marehemu Khatib Hassan Mzibondo, Nasra Juma Mohamed, wasanii Makame Faki Makame, Mwanacha Hassan Kijole,Maryam Mohammed Hamdani, marehemu Ali Salum Basalam.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top