BREKING NEWS, NECTA, WIZARA YA ELIMU ZANZIBAR ZATANGAZA MATOKEO YA MITIHANI

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imetangaza matokeo ya Darasa la sita, saba na kidatu cha pili ambapo ufaulu umeengezeka ukilinganishwa na matokeo ya mwaka uliopita.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma amesema,  Jumla ya watahiniwa 34,458 wamefaulu mitahani yao ya kidatu cha pili kati yao wanawake ni 20,793 na wanaume ni 13,665 ambapo ufaulu wao umeengezeka kwa asilimia 3.88% ukilinganisha na watahiniwa 17,581 sawa na asilima 70.1% kwa mwaka 2016.

Amesema katika matokeo hayo wanafunzi waliofanya mitihani yao kutoka darasa la sita jumla ya watahiniwa 15,098 wamefaulu kati yao wanawake 9,650 na wanaume 5,448  ambapo watahiniwa waliofanya mitahani yao kutoka darasa la saba jumla ya watahiniwa 19,360 wakiwemo wanawake 11,143 na wanaume 8,217 wamefaulu huku ufaulu wa wanafunzi wa kike uko juu ukilinganishwa na wanafunzi wa kiume.

Pia amesema ufaulu wa watahiniwa wa kidatu cha pili waliotoka darasa la saba ni mkubwa ukilinganishwa na ufaulu wa wanafunzi waliofanya mitihani yao kutoka  darasa la sita .

Akizungumzia kiwango cha kutofaulu kwa watahiniwa wa kidatu cha pili amesema jumla ya watahiniwa 12,122 hawakufaulu wakiwemo 5,789 waliofanya mitihani yao ya darasa la sita na 6,333 kutoka darasa la saba hivyo ni sawa na asilimia 26.02% ya wanafunzi ambao hawakufaulu.

Akizungumzia ufaulu wa wanafunzi wa darasa la  sita Waziri Pembe amesema jumla ya watahiniwa 31,145 sawa na asilimia 96.19 wamefaulu mitihani yao ya kuingia kidato cha kwanza mwaka 2018 kati yao Vipawa ni 138.

Amesema wanafunzi wa michipuo ni 1,387 sawa na asilimia 4.45 na waliondelea na masomo ya sekondari za kawaida ni 29,620 sawa na asilimia 95.11% ambapo ufaulu umeengezeka ukilinganishwa na watahiniwa wa mwaka 2016.

Amesema kwa matokeo hayo yanaonesha idadi ya watahiniwa wa vipawa imeengezeka kutoka 71 kwa mwaka 2016 hadi kufikia 138 kwa mwaka 2017 pia idadi ya watahiniwa waliofaulu kuingia michipuo imeengezeka kutoka 889 mwaka 2016 hadi kufikia 1,387 mwaka 2017.

Kwa upande wa darasa la nne Waziri Pembe amesema jumla ya watahiniwa 26,448 wamefaulu mitihani yao kati yao wanawake 14,764 na wanaume 11,684  ambapo ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 18.11% ukilinganishwa na watahiniwa 18,423 waliofaulu mwaka 2016. Aidha amesema kuwa watahiniwa 10,691 hawakufaulu mitihani yao ambapo idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na watahiniwa 16,258 kwa mwaka 2016.

Wakati huo huo Waziri Pembe amesema katika mitihani hiyo kulijitokeza kesi za udanganyifu ambapo watahiniwa wanane kutoka kidatu cha pili waligundulika kufanya udanganifu na kufutiwa matokeo yao kwa mujibu wa kanuni ya 58 (1) ya Baraza la Mitihani huku watahiniwa wa darasa la nne na la sita hawajafanya udanganyifu katika mitihani hiyo.

Hata hivyo amesema kuna baadhi ya wanafunzi hawajafanya mitihani kwa sababu mbali mbali ikiwemo Utoro, ugonjwa, kufariki na wengine kufunga ndoa.


KWA TAARIFA ZAIDI UNAWEZA KUTEMBELEA MTANDAO WA ww.necta.go.tz kwa matokeo ya kidato cha sita na matokeo ya kidato cha pili, darasa la sita na nne tembela www.moez.go.tz

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top