Kampala. Vikongwe Yakobo Rwakaikara (90) na Jane (82) wamefunga pingu za maisha Desemba 27,2017.

Wawili hao walikula kiapo cha ndoa katika Kanisa la St. James, Kigorobya wilayani Hoima.
Rwakaikara ni mwanaharakati wa zamani wa Chama cha NRM alichokisaidia kuendesha harakati za msituni ambako alipoteza watoto wake kadhaa.

Ndoa ilifungwa na Askofu mstaafu wa Jimbo la Bunyoro Kitara, Nathan Kyamanywa.
Katika mahubiri, askofu huyo alisema hakuna aliyechelewa kufuata misingi ya Mungu.

Aliwapongeza wanandoa hao kwa kuonyesha uvumilivu wakisubiri siku ya ahadi.



Askofu Kyamanywa amesema katika maisha yake ya uchungaji hakuwahi kufungisha ndoa ya watu wenye umri mkubwa kama huo, hivyo tukio hilo ni baraka kwake.

Pia, ametoa wito kwa familia kuwa na moyo wa upendo na uvumilivu ili kuwa na amani katika Taifa.

chanzo, Zanzibar 24

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top