Waziri wa Mazingira na Muungano,
January Makamba ameamua kutumia sehemu ya siku za mwisho wa mwaka
kuwakumbusha wenzake kuhusu nyadhifa wanazoshikilia.
“Uongozi ni koti la kuazima,” ameandika
waziri huyo wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika akaunti yake ya Twitter
jana, Kama ilivyo kwa watumaji wengi wa ujumbe mfupi katika mtandao huo,
Makamba hakutaka kufafanua kauli yake zaidi ya kuthibitisha kuwa iko
kwenye akaunti yake.
Makamba, mmoja wa makada walio katika
Baraza la Mawaziri la pili baada ya kuingia kwa mara ya kwanza wakati wa
utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne, ni mmoja wa watu wanaotuma ujumbe
mara kwa mara katika mtandao huo.
Katika ujumbe wa jana, Makamba
ameandika: “Uongozi ni koti la kuazima. Kuna wakati utarudisha tu. Kama
ulikuwa unawakoga nalo watu, likirudi unaadhirika.”
Pamoja na kutoa tahadhari hiyo, Makamba
bado hajakumbana na adha ya kupoteza uongozi tangu aondoke Ikulu ambako
alikuwa mwandishi wa hotuba wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne.
Baada ya kutoka Ikulu, mtoto huyo wa
katibu mkuu wa zamani wa CCM, aligombea ubunge wa Bumbuli mkoani Tanga
mwaka 2010 na kushinda na baadaye kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kabla ya kushika wadhifa wa sasa.
Hata hivyo, Makamba ameshuhudia mawaziri
wenzake kadhaa wakipoteza nyadhifa zao na kuwa wananchi wa kawaida,
wakiwamo walioenguliwa kutokana na kashfa kama za Tokomeza, Escrow,
makinikia, Tanzanite na wengine walioachwa katika mabadiliko ya kawaida
ya Baraza la Mawaziri.
Chanzo, Malunde
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment