NAIBU
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Abdalla Juma
Saadalla(Mabodi) amewahakikishia Umoja wa Vijana wa Chama hicho
(UVCCM) kuwa
ataendelea kushirikiana nao katika masuala mbali mbali ya kuwaletea
wananchi maendeleo.
Ahadi hiyo ameitoa wakati akizungumza na viongozi wa UVCCM
Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti Kheir James na Makamu Mwenyekiti Tabia Maulid
Mwita, waliofika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar
kwa ajili ya kutembelea na kuomba dua
katika kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya
Watu wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Aman Karume .
Dk. Mabodi aliwambia viongozi hao kwamba kumbukumbu na historia ya Marehemu Mzee Abeid karume
inatakiwa kulindwa na vijana wa CCM ambao wao ndio viongozi wa sasa na baadae
wenye dhamana ya kulinda serikali na
Chama visichukuliwe na wapinzani.
Naibu Katibu Mkuu huo amemtaja
Marehemu Mzee Abeid Karume kuwa
alikuwa ni kiongozi wa Mapinduzi mwenyekiti aliyekuwa na azna kubwa ya busara na falsafa pana ya masuala ya uongozi na
ubunifu ndani na nje ya ASP na Serikali kwa ujumla.
Amesema Afisi
Kuu ya CCM Zanzibar inayoongozwa na
Makamu Mwenyekiti Dk.Ali Mohamed Shein itatoa ushirikiano kwa UVCCM
pamoja na jumuiya na taasisi zote za kisiasa na kiserikali ili wananchi waendelee
kupata huduma bora za kijamii, kichumi na kisiasa.
Pia, ameueleza msafara
huo wa viongozi wa UVCCM waliofika Zanzibar kwa mara ya kwanza toka wachaguliwe
kupitia Mkutano Mkuu wa Tisa wa Umoja huo Taifa, kwamba maendeleo yaliyopatikana
visiwani Zanzibar yanatokana na juhudi za CCM kuisimamia Serikali itekeleze Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020.
“Kwanza karibuni sana Kisiwandui ambapo ndio sehemu pekee
yenye historia na Ofisi za waasisi wetu
wa Afro Shiraz Party (ASP), walioanzisha harakati za ukombozi wa Waafrika wa
visiwa vya Zanzibar na hatimaye Januari
12, 1964 wakaung’oa utawala wa kisultani na kusimamisha Dola huru iliyojali maisha na utu wa watu
wote.
Nyinyi vijana ni azna kubwa kwa chama chetu hivyo fanyeni
kazi kwa ufanisi ili kulinda heshima na dhamana mnazopewa kwa lengo la
kuwanufaisha vijana wenzenu ambao kwa
njia moja ama nyingine hawajajaliwa kama zenu”, alisema Dk.Mabodi.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM
Taifa , Kheir James amekipongeza
Chama cha Mapinduzi Zanzibar kwa juhudi zake za kuimarisha taasisi hiyo ya
kisiasa licha ya kuwepo na changamoto za kisiasa zinazosababishwa na wapinzani.
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment