BAKAR
Khamis (25) mkaazi wa Mitondooni Wilaya ya Wete, anadaiwa kumnajisi
(kumlawiti) mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne huko Shehia ya
Piki Wilaya hiyo.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi baba mzazi wa mtoto huyo alisema
mtuhumiwa alimchukuwa mwanawe hadi Bahanasa na kuingia kwenye gari ya
abiri na kumpeleka bonde la Hindi na kumfanyia ulawiti.
Alisema
mtuhumiwa ni mgeni katika shehia hiyo, alikwenda kwa kutembea, ingawa
alichokifanya ni kumchukua mtoto wake na kwenda kufanyia kitendo cha
ulawiti, jambo ambalo linamtia huzuni kila anapofikiria.
“Huyo
mtuhumiwa ni mgeni hapa kijijini kwetu, alipoona tu washamzoea watoto
ndipo alipoamua kumchukua mwanangu kwenda kumlawiti na huko kwao
tumesikia kaondoshwa kwa kuwafanyia watoto kitendo hicho”, alisema baba
huyo.
Kwa
upande wake mama wa mtoto, alisema aliondoka na kwenda mazikoni,
ambapo mara baada ya kufika alipigiwa simu na kuambiwa kuwa mwanae
amemfuata na ndipo alipofanya haraka ya kurudi, ingawa alipofika
hakumkuta.
“Alimpelea
katika bonde la Tangoni – Hindi na wakati anamlawiti wakatokea watoto
wanaochuma mabungo na mtuhumiwa akakimbia, ndipo walipomuuliza anapoishi
na kusema na wakamleta nyumbani”, alisema mama huyo.
Alieleza
mara baada ya kufika mtoto wao walimuhoji na kusema kuwa kaka Bakar,
alimchukua na kwenda kumfanyia kitendo cha ulawiti na kisha kumpa
maandazi, ambapo aliporudi alikuwa nayo kwenye mfuko.
“Walikuja
wazazi wa upande wa mtuhumiwa tufanye suluhu ili tusiifikishe kesi
Polisi, lakini kwa kitendo alichofanyiwa mwanangu siwezi kusamehe, kwani
huu ni ukatili”, alisema mama huyo.
“Huyu
mtoto ana kawaidi ya kucheza na mwanangu, sasa alikuja mwanangu na
kilio na kuniambia kaka ananikimbia, nikatoka nje nikamwita lakini na
mtuhumiwa ikawa anamwita, sasa ikawa kama tunavutiana, ingawa sikuwa na
wasiwasi nae nikaona labda anamfuata tu kwa vile washamzoea”, alisema
jirani wa mtoto huyo.
Nae,
kijana mmoja anaeishi mtaa huo, alisema alimshuhudia mtuhumiwa akiingia
kwenye gari na mtoto huyo maeneo ya Bahanasa na kuteremka Mzambarauni
majira ya saa 3:00, ingawa hakujua alikompeleka kutokana na yeye alikuwa
anaenda Wete.
“Mimi
sikufanya wasiwasi maana nilijua ni mdogo wake wa maduguni, kwa hiyo
niliporudi ndio nikapata taarifa hiyo na ndipo nilipokumbuka wakati
nilipomuona anapanda nae gari”, alisema kaka huyo.
Mratibu
wa shehia ya Piki, Bikombo Shazil Makame, alisema tukio hilo limetokea
katika shehia yake na tayari wameshalifikisha kituo cha Polisi Wete,
ambapo aliwataka wazazi kuwa mstari wa mbele kwenda kutoa ushahidi
mahakamani, ili kesi iweze kupata hatia.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji, alisema tukio hilo
lilitokea Januari 2 mwaka huu saa 6:00 mchana huko Piki, mtuhumiwa huyo
alimnajisi mtoto wa kiume mwenye miaka minne shehia ya Piki Wilaya ya
Wete.
Kamanda
huyo, alisema mtuhumiwa huyo ameshakamatwa na Jeshi hilo linaendelea na
upelelezi, ambapo watampeleka mahakamni mara baada ya uchunguzi
kukamilika kujibu tuhuma zinazomkabili.
Matukio
ya udhalilishaji kwa watoto ikiwemo ulawiti yamekuwa yakiongezeka kila
siku, kutokana na sababu mbali mbali, ikiwemo wanajamii kukataa kutoa
ushahidi pamoja na kesi kukaa muda mrefu mahakamani bila ya kupatiwa
hukumu.
Na Masanja Mabula -Pemba
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment