Polisi nchini Ureno wamemkamata
mwanaume mmoja kwenye uwanja wa ndege huko Lisbon, ambaye alikuwa amebeba kilo
moja ya cocaine kwenye makalio bandia.
Vyombo vya habari nchini humo
vilisema kuwa raia huyo wa Brazil aliwasili kwa ndege kutoka mji wa Belém do
Pará, kaskazini mwa Brazil.
Haijulikani ni vipi polisi
walifanikiwa kugundia hilo.
Mwanamume mwingine ambaye
anashukiwa kuwa angepokea dawa hizo alikamatwa kwenye kituo cha treni cha mji
huo.
Wanaume hao watakabiliwa na kesi
ya ulanguzi wa madawa ya kulevya.
Mwezi uliopita polisi nchini
Ureno na Uhispania walikamata cocaine ndani ya mananasi yaliyokuwa
yamessfirishwa kutoka Amerika ya Kusini.
Chanzo-
BBC
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment