Mvua kubwa iliyonyesha katika kijiji cha Mwekako kata ya Kasenga wilayani Chato mkoani Geita imesababisha vifo vya watoto wawili na kuharibu mali.
Diwani wa Kata ya Kasenga, Damian Vilarie amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema mvua imesababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara. 
Amesema mvua hiyo iliyonyesha kwa saa tatu jana Alhamisi Januari 11 ilisababisha mafuriko yaliyowasomba watoto wawili wa mzee Kurwa waliotoka soko la Igalula kununua bidhaa za nyumbani.
Amesema watoto hao mmoja anakadiriwa kuwa na miaka 13 na mdogo miaka mawili.
Na Rehema Matowo, Mwananchi

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top