Mbunge wa Geita, Joseph Msukuma amesema kwamba viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wanapiga kelele kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Lowassa kwenda Ikulu lakini hawana mabavu ya kumfukuza uanachama kwani yeye ndiye mwenye chama.
Msukuma amedai kwamba, Mbowe ambaye anaaminiwa kuwa ni Mwenyekiti wa
CHADEMA tayari alikwishauza chama kwa Lowassa muda mrefu ndiyo maana
hana sauti ya kumuwajibisha.
Aidha Msukuma hajaishia hapo ambapo pia amemtaka Mbowe ambaye ni
Mwenyekiti wa Chama hicho aoneshe nguvu yake ndani ya chama kwa
kumwambia Lowassa aombe radhi na siyo waombane wao kwa wao kwani
kutakuwa ni kuwapumbaza wanachama na wafusi wao bali hadharani watu
waone.
"Lowassa ndiye mwenye Chama. Wewe mbowe uliuza chama sasa wewe kama
msemaji toa kauli ya kumfukuza chama Lowassa. Tunashangaa kuanza
kuchafuliwa kwa mtu ambaye mlituaminisha kuwa anafaa kuwa Rais. Muite
Lowassa umhoji mitandaoni tuone akikuomba radhi. Na hata akikuomba radhi
sasa hivi tutajua siyo kwa mapenzi yake," Msukuma.
Kwa mujibu wa blog ya Malunde, Msuka ameongeza kuwa, "Mbowe kusema kuwa Lowassa alikurupuka ni kumkosea adabu
kwanza, Lowassa ni mtu mzima kwake na yeye bado ni kijana. Na
ninaamini kwamba wewe Mbowe Lowassa hakuombi msamaha kwa kuwa yeye ndiye
mmiliki".
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment