Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu nchini (HESLB) imesema kuanzia Jumatatu ijayo, Januari 8, 2017 itaanza kukagua taarifa za mishahara za waajiri (payroll) ili kubaini waajiri wao ambao wanawasilisha kiwango kidogo cha mikopo na wale wasiowasilisha kabisa pesa kwenye bodi na kuwachukulia hatua stahiki.

“Kuanzia Jumatatu, Jan. 8, 2017 tutaanza kukagua taarifa kwenye payroll za waajiri wote waliosajiriwa kubaini waajiriwa wao ambao ni wanufaika wa mikopo wanaodaiwa ili waweze kukatwa,” amesema Badru.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema wanufaika wengi wa mikopo, wakiwemo wadaiwa sugu, wameonesha ushirikiano mkubwa katika kurejesha mikopo yao, hivyo kurahisisha kazi ya kukusanya madeni ya mikopo hiyo.

“Tangu mwaka jana mpaka sasa tumewapata wadaiwa sugu 26,000, tunashukuru wanufaika hawa wamejitokeza na wanawasilisha mikopo yao ambapo ametaja kiasi cha pesa zinazodaiwa na wanufaika sugu wa mikopo na bado hakijaanzwa kurejeshwa ni Tsh. bilioni 285.

Hata hivyo, Badru amesema wamelazimika kufungua ofisi zao nchi nzima kwa ajili kusimamia malipo ya fedha hizo za mikopo, hasa wale waliotajwa kwenye orodha ya wadaiwa sugu.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top