Chama tawala nchini Burundi CNDD/FDD kimemtangaza Rais Pierre
Nkurunzinza kuwa kiongozi wa kudumu ndani ya chama hicho ambaye anaweza
kutawala milele.
Uamzi huo umefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa
chama hicho uliofanyika katika eneo la Buye alikozaliwa Rais Nkurunzinza
Kaskazini mwa nchi hiyo.
Aidha, uamuzi huo umechukuliwa wakati Burundi inajiandaa kufanya
marekebisho ya katiba ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea
kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.
Hata hivyo, Wanaharakati wa siasa nchini Burundi wanasema kuwa hatua
hiyo imezamilia kuua mjadala wa nani atakayemrithi rais katika uchaguzi
wa mwaka 2020.
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment