Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo, jamii, jinsia na Watoto, Dk Faustine
Ndugulile amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Afya akishirikiana na Taasisi
ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kufanya utafiti wa
afya ya uzazi kwa wanaume ili kubaini sababu za tatizo hilo na kujua
ongezeko la upungufu wa nguvu za kiume ni kubwa kiasi gani nchini.
Ndugulile
amefikia uamuzi huo kwani mara zote Serikali imekuwa ikitilia mkazo
afya ya uzazi kwa mwanamke na kusahau upande wa pili.
Amesema
kwa upande wa Tanzania mpaka sasa hakuna tafiti zozote zilizofanyika
juu ya tatizo hilo kwa wanaume, hivyo ni wakati wake sasa kulifanyia
uchunguzi wa kina na kubaini suluhusho lake.
Aidha
kwa tafiti zilizofanywa kisayansi duniani zimebaininsha kuwa wanaume
wengi wana matatizo ya nguvu za kiume sababu kubwa ikiwa ni mtindo wa
maisha, kwani wengi wao hupendelea kula vyakula ambavyo si bora vyenye
mafuta na sukari kwa wingi ambavyo kwa kiasi kikubwa huchangia magonjwa
yasiyoambukizwa na ukosefu wa nguvu za kiume.
Pia
tafiti hizo zimeonesha kwamba matumizi ya vilevi ikiwemo pombe na
sigara, kutofanya mazoezi mara kwa mara, unene kupita kiasi, msongo wa
mawazo, matumizi ya dawa kwa muda mrefu, magonjwa sugu kama kisukari na
presha kwa kiasi kikubwa huchangia tatizo hilo.
Katika
harakati za kupambana na tatizo hilo Serikali juzi imepitisha baadhi ya
dawa za tiba asili kutibu tatizo hilo ambazo zimethibitishwa na Mkemia
Mkuu na kuruhusiwa kutumika kukabiliana na tatizo hilo dawa hiyo ni
Ujana, huku dawa nyingine ambazo zimesajiliwa na zinafaa kutumiwa ni
Sildenafil na Tadalafil.
Dawa
hizo zimechunguzwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na
kuthibitishwa kuwa hazina sumu wala madhara kwa watumiaji na
zinapatikana katika maduka mbalimbali ya dawa.
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment