Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewafukuza kazi walimu 28 baada ya kugundulika kufanya ubadhirifu wa zaidi ya Shiling milion 100 fedha za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibra.
Amesema
uamuzi huo umekuja baada ya uhakiki katika wizara mbalimbali za
Serikali ya Zanzibar na kubaini kasoro ambazo watendaji wake walionekana
kufanya makosa hayo kwa makusdi.
Amesema
sababu za kufukuzwa kwa walimu hao ni kuchukua fedha za mishahara bila
ya kuwepo kazini kwa muda mrefu huku wakishindwa kabisa kutoa taarifa
kwa wahusika.
Mzee
amesema kwa mujibu wa takwimu zao katika uchunguzi huo zinaonyesha
watumisihi 46 wa Wizara ya Elimu visiwani hapa wamekuwa wakilipwa
mishahara bila ya kustahiki kulipwa fedha hizo.
“Kwa
mujibu wa takwimu zetu zinaonyesha kuwa watendaji waliokosa kuripoti
kazini kwa muda mrefu ni 20 wagonjwa 8 na 6 hawakujitokeza kabisa katika
uhakiki huo huku wengine wakishikiliwa kwa makosa mbalimbali.’’
Mzee kuwa amesema pamoja na kufukuzwa kazi walimu
hao waliokua wakichukua mishahara hewa lakini pia wanatakiwa kulipa
fedha hizo serikalini.
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment