Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Mhe. Mohamed Aboud Mohamed amewataka wafanyakazi wa Shirika la Bandari
Zanzibar kufanya kazi kwa bidii na kujenga uadilifu ili kuipatia pato zaidi Serikali
pamoja na kuleta maendeleo katika nchi.
Kauli hiyo
ameieleza leo huko katika ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Shirika la Bandari
Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya
sherehe ya miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Alisema
wafanyakazi waweze kupambana katika kuhakikisha wanazuia rushwa na
uingizaji wa biashara haramu jambo ambalo linaharibu nguvu kazi ya taifa na
kuipunguzia pato serikali .
“Lazima
wafanyakazi wadhibiti kuvuja mapato kama hakuna mapato katika serikali na
maendeleo hayapo na kipato hakiwi ikiwa kinatumiwa kwa ubadhirifu ” alisema
Waziri .
Aidha alisema
juhudi za serikali ni kutekeleza ilani ya chama ambayo inalengo la kuwaletea
maendeleo mbali mbali wananchi wake bila ya upendeleo na kusimamia utekelezaji
wa ahadi jambo ambalo ndio malengo makuu ya Mapinduzi .
Alifahamisha
serikali inatoa huduma kwa wananchi wote bila ya kuwa na ubaguzi wa rangi wala
jinsia yoyote katika sekta mbali mbali za serikali pamoja na njanja tofauti za
kisiasa kiuchumi na kijamii .
Alisema bandari
ndogo ndogo zina mtindo wa kupitisha biashara ya haramu ikiwemo madawa ya
kulevya na kutumia mbinu mbali mbali za kuichafua nchi hivyo alizitaka taasisi
husika kuchukua juhudi za kukabiliana nazo.
Alieleza kuwa
Zaidi ya Shilling Million 378 zilizotumika katika Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya
Shirika la Bandari la Mkokotoni na kuhakikisha kuwa si muda mrefu utaanza
ujenzi wa gati ambalo linatarajiwa liwe la kisasa lenye hadhi inayolingana na
mkoa huo.
Nae katibu Mkuu
wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe amesema ujenzi huu ni
utekelezaji wa ilani ya chama ambayo aliahidi Mheshimiwa Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ni moja ya ahadi
zake za kuhakikisha anaimarisha maendeleo ya miundo mbinu ya Mkoa
Kaskazini kwa kutekeleza ahadi mbali mbali ikiwemo ujenzi wa Ofisi
ya Bandari pamoja na Gati mpya ya mkokotoni ambayo inatarajia kuchukua
mizigo ya uzito wa tani mia moja.
Aidha alisema
ujenzi wa bandari hiyo inakusudiwa kutumia Zaidi ya Tsh,Bilioni
moja na Million 800 na gati hiyo inatarajiwa kuwa na urefu wa
mita 170 na upana wa mita sita bandari hiyo inasafirisha
abiria kwa kwenda na kurudi pamoja na mizigo mkaa mbao pamoja na dhamani .
Shirika la
Bandari lilianzishwa mwaka 1997 ikiwa ni muunganiko wa Idara mbili
ikiwemo Idara ya Bandari pamoja na Zanzibar Ofeji kwa lengo la kuleta
ufanisi na kuimarisha uchumi wa Zanzibar.
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment