|
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP
Simon Haule akionesha silaha aina ya AK-47 yenye namba 18116428 na
mafuta ya kulainishia silaha yaliyotupwa na majambazi waliotaka kuvamia
kiwanda cha Jielong.
|
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga
limefanikiwa kukamata silaha ya kivita aina ya AK-47 iliyotupwa na watu
wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa wanataka kuvamia kiwanda cha
kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd
kilichopo Nhelegani katika kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jana
Alhamis Januari 18,2018 Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon
Haule amesema walikamata silaha hiyo usiku wa kuamkia leo majira ya saa
tano eneo la Tinde wakati majambazi hao wanafuatiliwa na polisi ndipo
wakaamua kutupa bunduki hiyo.
“Silaha hii aina ya AK-47 yenye namba
18116428 ilikuwa imefungwa kwenye skafu yenye rangi ya nembo ya Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiwa na risasi 25 ndani ya
magazine yake na risasi zingine 8,zikiwa kwenye mfuko mdogo wa
nailoni”,alieleza Kamanda Haule.
|
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP
Simon Haule akionesha bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428
iliyotupwa na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Jielong
|
“Majambazi wawili pia walitelekeza pikipiki aina ya SANLG yenye namba
za usajili MC 856 BPF,mafuta ya cherehani ya kulainishia silaha,tochi
mbili na koti zito”,aliongeza.
Alisema jeshi la polisi lilipata taarifa za majambazi hao kutaka kuvamia
kiwanda hicho kinachomilikiwa na raia wa China tangu tarehe 6.01.2018
kisha kuanza kuwafuatilia na kubaini kuwa baadhi yao ni wakazi wa
Kahama na Ushirombo ambapo amewataka kujisalimisha polisi.
Na Kadama Malunde
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP
Simon Haule akionesha pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili MC
856 BPF iliyotelekezwa na majambazi
Facebook Blogger Plugin by
Piere
Post a Comment