Jeshi la polisi Tanzania wakishirikiana na jeshi la polisi la Msumbiji leo Januari 15, 2018  wamesaini mkataba wa mashirikiano ya ulinzi na usalama baina ya Nchi hizo mbili ili kudhibiti na kokomesha uhalifu mipakani sambamba na kukomesha uhamiaji haramu.

 

Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dar es salam katika ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania ambapo IGP Sirro amesema,  mkataba huo wa mashirikiano ya ulinzi utasaidia kutunza na kudumisha amani kutokana na mashirikiano hayo.

 

Aidha IGP Sirro ameongelea mapigano ya majambazi ambao walikuwa wakipambana nao kibiti walikimbilia msumbiji na muungano huo utaleta mafanikio na kuwataka wote ambao wapo nchi msumbiji kuwa popote watakapo kimbilia bado hawatakuwa salama.

 

Kwa upande wake IGP Bernadino Rafael wa Msumbiji amesema makubaliano hayo yatawasaidia kuimarisha ulinzi na  kubadilishana na kujifunza mbinu mbalimbali ambazo jeshi la polisi la Tanzania wamekua wakizitumia ili kudhibiti uhalifu  na pia izi utazidi kuwa imara,  na madhaifu madhaifu ya polisi wa Tanzania,Zanzibar 24

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top